Morocco vs Tanzania leo – Saa, chaneli, vikosi na hali ya kundi (AFCON 2025)
Morocco vs Tanzania leo AFCON 2025: Saa ya mchezo, wapi kutazama moja kwa moja, vikosi vinavyotarajiwa na nafasi ya Taifa Stars katika hatua ya 16 bora.
Leo ni siku ya kihistoria kwa Taifa Stars. Tanzania inakutana na Morocco katika hatua ya 16 bora ya AFCON 2025, ikiwa ni mara ya kwanza kufika hatua hii tangu ilipoanza kushiriki mashindano haya. Morocco, ikiwa mwenyeji na moja ya timu bora Afrika, ni mpinzani mgumu. Lakini Taifa Stars wapo tayari kupambana.
- Mchezo unachezwa wapi
- Wapi kutazama mechi moja kwa moja
- Vikosi vinavyotarajiwa kuanza
- Hali ya kila timu
- Matokeo ya Moja kwa Moja
- Hali ya kundi – Nafasi ya Taifa Stars
Mchezo unachezwa wapi
- Uwanja: Prince Moulay Abdellah, Rabat (Morocco)
- Tarehe: Alhamisi, 04 Januari 2026
- Muda: Saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania (19:00 EAT - 17:00 CET)
Wapi kutazama mechi moja kwa moja
Mashabiki wa Tanzania wanaweza kutazama mechi hiyo kupitia Azam TV na DStv (SuperSport), ambazo zote zitarusha moja kwa moja. Kwa wale wanaopenda matangazo ya ndani, TBC pia inatarajiwa kurusha mchezo huo. Kimataifa, Morocco dhidi ya Tanzania itaonyeshwa kwenye beIN Sports, Claro Sports (YouTube), na Movistar+ katika sehemu mbalimbali za dunia.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza
Morocco (4-2-3-1)
- Kipa: Bono
- Mabeki: Mazraoui, Aguerd, El Yamiq, Salah-Eddine
- Viungo: Amrabat, Ounahi, El Aynaoui
- Washambuliaji: Saibari, Brahim Díaz, El Kaabi
Tanzania (4-2-3-1)
- Kipa: Masaranga
- Mabeki: Mohamed Hussein, Hamad, Mwamnyeto, Job
- Viungo: Miroshi, Msanga
- Washambuliaji: Msuva, Feisal, Mnoga
- Mshambuliaji wa mbele: Mbwana Samatta
Hakuna majeruhi waliothibitishwa hadi sasa na makocha wote wanatarajiwa kutegemea nyota wao waliowezesha kufuzu hatua hii.

Hali ya kila timu
Morocco wamekuwa kwenye kiwango bora: waliongoza Kundi A bila kupoteza mchezo (ushindi 2, sare 1). Wanajivunia wachezaji wanaocheza Ulaya, safu imara ya ulinzi, na faida ya kucheza nyumbani. Hata hivyo, wanakabiliwa na presha kubwa ya kutwaa ubingwa mbele ya mashabiki wao.
Tanzania, licha ya kutopata ushindi hatua ya makundi, walipambana kwa sare dhidi ya Tunisia na Uganda, na kupoteza kwa Nigeria. Kwa alama 2, walifuzu kama mojawapo ya timu bora za nafasi ya tatu. Kikosi kiko na morali ya juu na hamasa kubwa ya kufanya historia zaidi.
⏰Matokeo ya Moja kwa Moja – Morocco vs Tanzania
Sehemu hii itasasishwa moja kwa moja wakati mechi ikiendelea.
Hali ya kundi – Nafasi ya Taifa Stars
Tanzania ilimaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya 3 katika Kundi C, nyuma ya Nigeria na Tunisia. Kwa alama 2 (sare mbili, kichapo kimoja), waliingia 16 bora kama mmoja wa “best third-placed teams”.

Kundi C lilivyomalizika:
- Nigeria – 9 pts
- Tunisia – 4 pts
- Tanzania – 2 pts
- Uganda – 1 pt
Hii ni hatua kubwa kwa soka la Tanzania. Ushindi dhidi ya Morocco leo utawaweka katika robo fainali kwa mara ya kwanza kabisa.